MAAFA YARIPOTIWA KWENYE MAANDAMANO MOROCCO
Watu wasiopungua 2 wameuawa kwenye maandamano yanayoongozwa na vijana wa kizazi cha Gen Z nchini Morocco, haya yakiwa mauaji ya kwanza kuripotiwa tangu kuzuka kwa maandamano kote nchini humo Jumamosi.
Waandamanaji wameghadhabishwa na hatua ya serikali kujenga viwanja vya mpira wa soka katika maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia, badala ya kuboresha huduma kwa wananchi kama vile hospitali na hali ya uchumi.
Maandamano yamekuwa yakifanywa usiku, huku kundi la Gen Z 212 ambalo limeandaa maandamano hayo likijetenga na jaribio la kuvamia kituo cha polisi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































