#uncategorized

KENYA YAONGOZA KWA DHAHABU JAPAN, TANZANIA WAFUATA

Wanariadha Abraham Kibowott na Edmund Serem watapeperusha bendera ya Kenya hii leo katika mashindano ya ubingwa wa riadha ulimwenguni jijini Tokyo Japan, watakapoingia uwanjani kushiriki mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwa wanaume.

Mbio hizo zitaanza majira ya 3:55pm saa za Afrika Mashariki, wakenya wakikabiliwa na ushindani kutoka kwa wenzao Lamecha Girma wa Ethiopia na Soufiane El Bakkali wa Morocco.

Kenya inaongoza kwa nishani za dhabau barani Afrika katiika mashindano hayo yaliyoanza Jumamosi, ikiwa na dhahabu 2 kupitia kwa Beatrice Chebet katika mbio za mita 10,000 na Peres Jepchirchir katika mbio za marathon.

Tanzania imepata dhahabu yake ya kwanza kabisa mapema leo kupitia kwa Alphonce Felix Simbu aliyeonyesha ubabe mwishoni mwa mbio hizo na kumpiku Amanal Petros wa Ujerumani katika mbio za marathon.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KENYA YAONGOZA KWA DHAHABU JAPAN, TANZANIA WAFUATA

GACHAGUA ATANGAZA AZMA YA URAIS

KENYA YAONGOZA KWA DHAHABU JAPAN, TANZANIA WAFUATA

KCB RFC WATAWAZWA MABINGWA WA DALA 7S,

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *