RAIS RUTO AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA TURKANA
Rais William Ruto ameendeleza vikao vyake vya mara kwa mara na viongozi wa mashinani kutoka maeneo mbali mbali nchini, ambako analenga kuwafahamisha kuhusu utendakazi wa serikali yake na miradi ya maendeleo ambayo serikali yake imetekeleza katika maeneo hayo.
Mapema leo, rais amekutana na viongozi wa mashinani kutoka kaunti ya Murang’a, muda mfupi baada ya kuwaalika viongozi wa kaunti ya Turkana.
Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho cha Ikulu ni Pamoja na naibu rais Kithure Kindiki, mawaziri, wabunge na wawakilishi wadi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































