MARAGA ATAKA POLISI WAFUNZWE KUHUSU HAKI
Pana dharura ya kuwapa maafisa wa polisi mafunzo kuhusu haki za kimsingi za kibinadamu ili kukabili ukiukaji wa haki hizo wakati wa maandamano nchini.
Ni kauli ya aliyekuwa jaji mkuu David Maraga, akizungumza kwenye mahojiano na runinga moja nchini, ambako amekosoa hatua ya polisi kumrushia vitoza machozi alipojitokeza kudai haki kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao mikononi mwa polisi.
Aidha, amepuzilia mbali michango ya fedha inyoendelezwa na serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































