#Local News

DCI YAKAMATA KIJANA ALIYEDHALILISHA BENDERA YA TAIFA NYAYO

Maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi, DCI, wamemkamata kijana mwenye umri wa miaka 17 aliyetambuliwa kupitia video inayosambaa mitandaoni, akiharibu bendera ya taifa wakati wa mechi ya kandanda katika uwanja wa Nyayo.

Tukio hilo limezua hasira miongoni mwa Wakenya wengi, huku viongozi wa usalama wakilaani vikali kitendo hicho na kukitaja kama kosa linalodhalilisha heshima ya taifa.

Kijana huyo kwa jina Ibrahim Haidar Yusuf anatarajiwa kufikishwa mahakamani ambapo atashtakiwa kwa makosa yanayohusiana na kudhalilisha alama za taifa huku polisi wakiwatafuta washukiwa wengine.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

DCI YAKAMATA KIJANA ALIYEDHALILISHA BENDERA YA TAIFA NYAYO

UBOVU WA BARABARA WAWAHAMISHA WAKAZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *