SHULE ZATISHIA KUWAREJESHA WANAFUNZI NYUMBANI
Wakuu wa shule za upili nchini wameonya kuhusu uwezekano wa masomo kutatizika muhula huu wa mwisho kutokana na ukosefu wa fedha za kufanikisha uendeshaji wa shughuli shuleni.
Kulingana na wakuu hao, serikali haijatuma asilimia 20 iliyosalia ya mgao wa shule, na huenda wakalazimika kuwarejesha nyumbani wanafunzi.
Sera ya mgao wa masomo inaishinikiza serikali kutoa asilimia 50 ya mgao kwa muhula wa kwanza, asilimia 30 muhula wa pili huku asilimia 20 muhula wa mwisho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































