ZAIDI YA MILIONI 26 WAKO SHA- DUALE
Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 59.3 kwa hospitali mbali mbali kupitia bima ya afya ya jamii SHIF kufikia sasa.
Haya ni kulingana na Waziri wa afya Aden Duale, akisema bilioni 29.8 kati ya fedha hizo zimetumwa kwa hospitali za kibinafsi, zile za kaunti zikipokea bilioni 13.7, nyingine zikitumwa kwa hospitali za kitaifa na za kimisheni.
Aidha, amesema wakenya zaidi ya milioni 26 wamesajiliwa kwenye mamlaka ya SHA huku serikali ikiusanya zaidi ya shilingi bilioni 70 kupitia ada wanazolipa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































