BARASA AMKOSOA UHURU
Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa amekosoa madai ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwamba serikali ya Kenya Kwanza inaporomosha mafanikio ya utawala wake.
Akizungumza katika eneo la Navakholo Kaunti ya Kakamega, Barasa amesema kwamba Kaunti ya Kakamega haikupata miradi mikubwa yoyote chini ya uongozi wa Kenyatta na kumtaka Rais Mstaafu kuwacha uongozi wa Serikali ya Kenya kwanza utumikie wakenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































