GACHAGUA AKATIZA ZIARA MAREKANI
Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua ametangaza kukatiza ghafla zira yake nchini Marekani, akisema analenga kurejea nchini ili kujiunga na chama chake cha DCP katika maandalizi ya chaguzi ndogo zilizoratibiwa mwezi Novemba mwaka huu.
Kupitia taarifa, Gachagua amesema hatafauli kuhudhuria vikao vilivyokuwa vimepangwa nchini humo, akisema vikao vilivyosalia vinaweza kupangwa tena mapema mwaka ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































