#Local News

E-GP SI TAFADHALI, RUTO AONYA

Rais William Ruto amesisitiza kuwa mfumo wa utoaji zabuni za serikali kwa njia ya kielektroniki yaani e-Procurement ni lazima, licha ya pingamizi kutoka kwa viongozi mbali mbali wakiwemo magavana na maseneta wanaosema shughuli za kaunti zimekwama kutokana na mfumo huo.

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto amewakosoa wanaopinga mfumo huo, anaoutaja kuwa wenye kuhakikisha uwazi katika utumiaji wa fedha za mlipa ushuru.

Kulingana na wanaopinga, mfumo huo unachelewesha usambazaji wa vifaa kwa kaunti.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

E-GP SI TAFADHALI, RUTO AONYA

FAINALI YA DALA SEVENS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *