#Local News

MWANGI KUFIKA MAHAKAMANI KAHAWA

Mwanaharakati wa humu nchini Boniface Mwangi ameratibiwa kufikishwa katika mahakama ya Kahawa jijini Nairobi ambako atafunguliwa mashtaka ambayo polisi wameyataja kuwa yanayohusiana na ugaidi.

Mwangi alikamatwa siku ya Jumamosi nyumbani kwake kwenye kaunti ya Machakos kabla ya kusindikizwa hadi afisi yake jijini Nairobi ambako polisi wanasema walipata risasi bandia, vitoza machozi 2 ambavyo havijatumika miongoni mwa vifaa vingine.

Kulingana na idara ya upelelezi wa jinai DCI, Mwangi alihusika katika kupanga na kufadhili matukio ya kigaidi wakati wa maandamano ya tarehe 25 mwezi jana, wanaharakati wakipinga madai hayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWANGI KUFIKA MAHAKAMANI KAHAWA

RAILA: NIKO NA RUTO HADI 2027

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *