KENYA NDANI YA ROBO FAINALI
Kenya Harambee Stars ilijikatia tikiti ya robo-fainali katika Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 baada ya mabingwa mara mbili wa CHAN wa CHAN DRC congo kuwalambisha kivimbi Angola kwa mabao 2-0 huku Morocco ikiifunga Zambia mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa wa Nyayo
Ushindi huo wawili ulihakikisha kuwa, huku kukiwa na mchezo mmoja uliosalia kuchezwa, Kenya haiwezi kupitwa tena kwa kumaliza katika kundi la pili.
Harambee Stars wako kileleni mwa Kundi “A” kwa alama saba kutoka kwa mechi tatu baada ya kuzishinda DR Congo na Morocco 1-0 na kutoka sare na Angola.
Morocco na DR Congo pia wana pointi sita, Angola wana pointi nne na wametolewa, na Zambia bado hawajashinda.
Kulingana na sheria za CHAN, timu mbili za juu katika kila kundi zinafuzu kwa robo fainali. Hata kama watapoteza mchezo wa mwisho wa kundi dhidi ya Zambia siku ya Jumapili, makali yao ya dhidi ya DR Congo na Morocco yanawahakikishia kufuzu inavyofahamika kw akimombo kama head to head.
Kenya iko salama kwa kuwa tayari wamezishinda DR Congo na Morocco.
Kenya itamenyana na Zambia katika mchezo ambao sasa ni wa kawaida tu wa kufuzu lakini mchezo utakaoamua nafasi za mwisho za kundi.
Wakati huo huo, Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pia zitachuana katika kile ambacho ni sawa na mchuano wa mshindi wa kuwania nafasi iliyosalia ya robo fainali kutoka Kundi “A”.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































