WASHUKIWA ‘WALIOCHOMA VITUO VYA POLISI KUFAHAMU KESI JUMANNE
Washukiwa 6 wanaotuhumiwa na mashtaka ya kuteketeza kituo cha polisi cha Matuu na wengine 16 wanaokabiliwa na tuhuma za kuteketeza kituo cha polisi cha Makongeni watafahamu hatma ya kesi dhidi yao Jumanne wiki ijayo.
Hii ni baada ya upande wa mashtaka kuiambia mahakama kwamba ungali kukamilisha uchunguzi, na kwamba unalenga kufanyia marekebisho baadhi ya mashtaka.
Hata hivyo, mawakili wa washtakiwa wameukosoa upande wa mashtaka kwa madai ya kutumia kizingiti cha kutokamilika kwa uchunguzi ili kuhujumu utoaji haki.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































