MTOTO WA MIAKA 6 ATEKETEA KAKAMEGA
Polisi katika kaunti ya Kakamega wanachunguza kisa ambapo mvulana mwenye umri wa miaka 6 ameteketea hadi kufa katika nyumba yao mtaani Bukura eneo bunge la Lurambi.
Wakazi wamesema mamake mwathiriwa alimwacha mvulana huyo katika nyumba hiyo na kuelekea katika soko la Bukura kwa biashara zake za kila siku kabla ya kufahamishwa kuhusu kuteketea kwa nyumba yake.
Mwili wa mvulana huyo umepelekwa katika hifadhi ya maiti kwenye hospitali ya rufaa mjini Kakamega.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































