KESI YA REX KUENDELEA LEO
Uchunguzi katika mauaji ya mwanarika la Gen Z Rex Maasai umeratibiwa kuendelea hii leo mahakamani baada ya kikao hicho kuahirishwa hapo jana kufuatia hatua ya upande wa mashtaka kuishtumu idara ya polisi kwa madai ya kupuuza maagizo ya mahakama.
Hii ni baada ya idara hiyo kukosa kuwasilisha kwa muda mwafaka rekodi zinazoonyesha jinsi maafisa wa polisi huchukua na kurejesha bunduki vituoni.
Rekodi hiyo iliwasilishwa baadaye ila upande wa mashtaka ukaomba muda wa kuipekua kabla ya kesi kuendelea.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































