IEBC YALALAMIKIA UKOSEFU WA FEDHA
Chaguzi ndogo 8 zinazotarajiwa kuandaliwa mwezi Novemba mwaka huu ziko katika hatari ya kuahirishwa kutokana na ukosefu wa fedha za kufanikisha maandalizi ya chaguzi hizo.
Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya uhasibu katika bunge la kitaifa, mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Erastus Ethekon, amesema hazina ya kitaifa haijatoa fedha za kutosha, akisema shilingi bilioni 1 zinahitajika kuandaa chaguzi zote 24.
Ameongeza kuwa IEBC inalenga kufikisha wapiga kura milioni 29 kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































