GAMBIA YAWASILI TAYARI KUMENYANA NA STARS
Timu ya taifa ya kandanda ya Gambia imewasili nchini Kenya ikijiandaa na mechi muhimu ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026 dhidi ya Harambee Stars, itakayochezwa Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi, Kasarani, Nairobi.
Akizungumza na vyombo vya habari katika uwanja wa Kasarani Annex II, kocha mkuu wa Gambia na kocha wa zamani wa Gor Mahia, Jonathan McKinstry, alionyesha imani na kikosi chake lakini akakiri changamoto iliyo mbele yao.McKinstry aliitaja mechi hiyo kuwa muhimu sana kwao, akijua haitakuwa rahisi kwa sababu wanacheza ugenini, katika uwanja wa nyumbani wa Kenya.
Pia, alitaja uungwaji mkono mkubwa wa Harambee Stars wa nyumbani ambao ulianza wakati wa Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) kuwa sababu ya wasiwasi mkubwa wanapojiandaa kumenyana na Kenya.
Pia alibainisha kuwa wachezaji wengi wa sasa wa Harambee Stars wanafahamika kwake tangu alipokuwa akifundisha Gor Mahia FC; aliwafunza wachezaji wao kadhaa nchini Kenya, hivyo anajua uwezo wao.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































