UASU, KUSU KIBABII WAGOMA
Mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma umelemaza masomo katika vyuo hivyo kwa siku ya pili, wahadhiri wakishinikiza kutekelezwa kwa mkataba wao na serikali kabla ya kurejea kazini.
Katika kaunti ya Bungoma, wahadhiri wa chuo kikuu cha Kibabii wamejiunga na wenzao kote nchini, wakisema serikali imekuwa ikiwahadaa kurejea kazini ila inakosa kutekeleza makubaliano.
Wafanyakazi wa chuo hicho chini ya muungano wa KUSU pia wamegoma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































