WANAFUNZI WATISHIA KUJIUNGA NA WAHADHIRI KUGOMA
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma wametishia kujiunga na wahadhiri wao katika mgomo wa kitaifa iwapo serikali haitatua mgomo wa wahadhiri kufikia leo.
Kulingana na wanafunzi hao, mgomo huo ambao umeingia wiki ya 3 umewaacha bila cha kufanya mbali na kukosa kufundishwa, wakihofia kwamba huenda ukaathiri kalenda ya masomo.
Wahadhiri wanashinikiza serikali iwalipe shilingi bilioni 7.9 za makubaliano ya mwaka 2017-21.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































