KILABU YA 3K YAIMAIRISHA MAANDALIZI YA MSIMU UJAO
Klabu ya 3K ya Ligi ya Kitaifa ya Super League (NSL) imeimarisha maandalizi yao ya msimu ujao kwa kusajili wachezaji wapya na mfululizo wa mechi za kirafiki kupangwa ili kuimarisha utimamu wao.
kocha msaidizi wa klabu hiyo Moses Munene amethibitisha kwamba klabu hiyo tayari imewakamata Titus Kapchanga kutoka kwa Ligi Kuu ya FKF ya Murang’a SEAL na Salasya Otieno kutoka Juja Sporting, miongoni mwa wachezaji wengine waliosajiliwa.
Wakati huo huo, kilabu kimeachana na wachezaji kadhaa wakiwemo Lary Odhiambo ambaye amejiunga na MCF, Joshua Amunike amehamia Kabati Youth, huku Onesjuma Juma akisajiliwa na timu ya Daraja la Kwanza ya Compel FC.
Mshambulizi wao mahiri, Michael Macharia, yuko mbioni kutimkia Murang’a SEAL, huku Michael Owen akivutia pia timu ya daraja la juu Talanta FC.
Licha ya kuondoka, Munene alishikilia kuwa timu inasalia imara, akibainisha kuwa ni mchezaji mmoja pekee kutoka kwa wachezaji wa kawaida wa kuanzia kumi na moja msimu uliopita aliyesalia.
Timu hiyo pia imepanga mechi za maandalizi ili kutathmini ufaafu na ushirikiano wa wachezaji wapya waliosajiliwa kabla ya kampeni ya NSL kuanza.
Kikosi hicho kitakuwa kinasaka kuwa na kampeni yenye mafanikio kwa lengo la kujishindia daraja la Ligi Kuu ya FKF baada ya kukosa msimu uliopita.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































