SIKU YA GAVANA MUTAI SENETI
Gavana wa Kericho Erick Mutai anatazamiwa kufahamu hii leo iwapo ataendelea kuwa gavana au la, kwenye uamuzi utakaotolewa kupitia kura ya maseneta ikiwa ni siku ya 3 na ya mwisho ya kusikiliza hoja ya kubanduliwa kwake.
Wawakilishi wadi wa kaunti hiyo wameendelea kuishawishi seneti kudumisha uamuzi wao wa kumbandua, wakidai kwamba amefuja fedha za umma.
Hata hivyo, Mutai amejitetea akisema mfumo uliotumiwa kupiga kura ya kumtimua ulikumbwa na dosari, spika Amason Kingi akiagiza uchunguzi kwenye mfumo huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































