#uncategorized

SHIKANGWA AFANYA MAZOEZI ULAYA BAADA YA KUACHANA NA SIMBA SC

Mshambulizi wa Harambee Starlets, Jentrix Shikangwa Milimu anasema uamuzi wake wa kuachana na wababe wa soka ya wanawake ya Tanzania, Simba Queens, umechochewa na nia ya kutafuta changamoto mpya.

Shikangwa aliachana na timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi wiki moja iliyopita na kuashiria mwisho wa sura nzuri katika soka la wanawake Tanzania.

Shikangwa alikuwa miongoni mwa wachezaji 11 walioachwa na Simba, orodha hiyo ni pamoja na beki wa Harambee Starlets Wincate Kaari.

Shikangwa alijiunga na Simba Queens Januari 2024 baada ya kusaini mkataba mfupi wa miezi sita na timu ya Asia, Beijing Professional, nchini China, na kuacha historia nzuri. Msimu wa 2024-25, alikuwa mfungaji bora wa klabu hiyo, akifunga mabao 24 na kuisaidia Simba Queens kumaliza kama washindi wa pili wa ligi.

Kimataifa, Shikangwa anasalia kuwa nguzo muhimu katika uundaji wa Harambee Starlets, ingawa alitatizika kwa dakika chache katika mechi ya hivi majuzi ya Cecafa.

Mafanikio yake ya nyumbani nchini Kenya pia ni ya kupigiwa mfano, baada ya kushinda mara 3 taji la Ligi Kuu ya Wanawake ya FKF (2017, 2018, na 2019), akiwa na Vihiga Queens.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SHIKANGWA AFANYA MAZOEZI ULAYA BAADA YA KUACHANA NA SIMBA SC

KENYA YAIDHINISHWA KUANDAA CHAN

SHIKANGWA AFANYA MAZOEZI ULAYA BAADA YA KUACHANA NA SIMBA SC

GYOKERES BADO ANAWINDWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *