#Local News

SAKAJA APONEA MJELEDI WA BUNGE

Ni afueni kwa gavana wa Nairobi Johnson Sakaja baada ya wawakilishi wadi katika bunge la kaunti hiyo kusitisha kwa muda wa siku 30 mchakato wa kumbandua kutoka mamlakani waliokuwa wameanzisha.

Hii ni kufuatia wito wa Rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga kwa wawakilishi wadi hao, katika mikutano miwili tofauti ambako viongozi hao wamearifiwa kuwaomba wawakilishi wadi kushirikiana na gavana Sakaja ili kuwatumikia wakazi.

Wawakilishi walikuwa wakilalamikia masuala kadhaa ikiwemo utaratibu wa miradi ya maendeleo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SAKAJA APONEA MJELEDI WA BUNGE

WAHUDUMU WA UHC WAPATA AFUENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *