MGOMO WA WAHADHIRI WANG’ATA VYUO VIKUU
Athari za mgomo wa wahadhiri zimeanza kujitokeza kwa siku ya 3 sasa, wanafunzi wakikosa kuanza masomo yao kwa muhula huu jinsi walivyokuwa wametarajia huku wahadhiri wakishikilia kuwa hawatarejea kazini hadi malalamishi yao yashughulikiwe.
Wahadhiri wanashinikiza kutekelezwa kwa makubaliano yao na serikali, kwenye mkataba wa mwaka 2021-25 waliotia Saini na serikali.
Hata hivyo, Waziri wa elimu Julius Ogamba amewahimiza kurejea kazini, akisema serikali imeanza kutekeleza makubaliano hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































