WANYAMA APONGEZA HARAMBEE STARS
Nahodha wa zamani wa Harambee Stars Victor Wanyama amepongeza timu ya taifa ya kandanda Harambee Stars kwa uchezaji wao katika michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) inayoendelea.
Akiongea wakati wa ziara ya kuwania taji la CHAN, Wanyama alisema mengi yameboreka katika mtindo wa uchezaji wa timu ya taifa tangu Benni McCarthy achukue usukani.
Licha ya kutolewa kwenye hatua ya robo fainali na Madagascar, Wanyama anaamini kuwa timu hiyo inaelekea katika njia sahihi.
Huku CHAN ikiwaruhusu wachezaji wa ndani pekee kuwakilisha nchi zao, mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya alisema utendaji wa Stars katika michuano hiyo unaonyesha jinsi ligi ya Kenya inavyoweza kuwa na ushindani ikiwa uwekezaji ufaao utafanywa, kama ilivyoshuhudiwa wakati wa mashindano.
Kiungo huyo wa zamani wa Tottenham aliendelea kuwatia moyo wachezaji waliokosa penalti ambazo ziliifanya Stars kutolewa nje kwa Chin na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha katika kampeni zijazo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































