DEMBELE ASHINDA TUZO LA BALLON D’OR
Fowadi wa Ufaransa Ousmane Dembele alishinda tuzo ya Ballon d’Or kwa wanaume katika hafla iliyofanyika Paris hapo jana
Hili ni tuzo la mtu binafsi lenye hadhi zaidi katika kandanda likituzwa kwa nafasi yake katika kikosi cha Paris Saint-Germain kilichoshinda Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
Dembele, 28, alimshinda mchezaji wa Barcelona na Uhispania Lamine Yamal kwenye tuzo na kumrithi kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Rodri, ambaye alishinda kombe hilo mnamo 2024.
Mshambulizi wa Arsenal Viktor Gyokeres alishinda tuzo ya Mshambuliaji Bora kwa ushujaa wake msimu uliopita huku akiwa na Sporting Lisbon ya Ureno, Gianluigi Donnarumma alishinda tuzo ya Kipa Bora huku Meneja wa PSG Luis Enrique akitwaa tuzo ya Kocha Bora.
Winga huyo wa zamani wa Borussia Dortmund na Barcelona, ambaye alikuwa sehemu ya timu ya Ufaransa iliyoshinda Kombe la Dunia mwaka 2018, alifunga mabao 35 katika michuano yote huku PSG ikishinda ligi ya Ufaransa na vikombe maradufu pamoja na Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Yamal mwenye umri wa miaka 18, ambaye alikuwa mchezaji mwenza wa Dembele katika Barcelona aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa 202 mapema kabla ya kushinda 202. 21 – mwaka wa pili mbio ametwaa tuzo hiyo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































