MGOMO WA MADAKTARI KULEMAZA MATIBABU
Wakenya wanakabiliwa na hatari ya kukosa huduma za matibabu katika hospitali za umma iwapo serikali haitatekeleza matakwa ya madaktari ikiwemo nyongeza ya mishahara ndani ya muda wa siku 14 zijazo.
Wakitoa tangazo hilo, madaktari kupitia kwa katibu mkuu wa muungano wao Dakta Davji Atellah wameikosoa serikali kwa walichokitaja kama ukiukaji wa wazi wa mkataba wa maelewano wa kati ya mwaka 2017-2021.
Malalamishi mengine ni kutolipwa malimbikizi yao jinsi walivyokubaliana kwenye mkataba uliositisha mgomo wa mwaka jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































