AFISA WA KENYA AUAWA HAITI
Maafisa wa polisi wanane wa vikosi vya usalama vya Pamoja nchini Haiti akiwemo afisa wa Kenya wamejeruhiwa vibaya baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani ambako afisa huyo wa Kenya amefariki dunia kutokana na ajali hiyo.
Kulingana na msemaji wa operesheni hiyo, Jack Ombaka tukio hilo lilitendeka majira ya saa 5 jioni wakiwa kazini ambako magari yao mawili yaliyokuwa yakikokotana yalipata matatizo ya kiufundi kabla ya kugongana.
Afisa huyo alifariki alipkuwa akitibiwa katika hospitali ya Lambert Sante jijiini Petion-ville alikokuwa amepelekwa Pamoja na maafisa wenza na raia waliojeruhiwa.
Hata hivyo, maafisa watatu wako katika hali mbaya na wameratibiwa kuhamishwa katika hospitali nchini Dominican Republic kwa matibabu maalum, huku familia ya afisa aliyefariki ijifahamishwa.
Kkundi Cha MSS, kinachoongozwa na Kenya, kilipelekwa Haiti mwaka mmoja uliopita na hata hali imezidi kuwa mbaya, katikati mwa Jiji la port-au-Prince likiwa chini ya udhibiti wa genge.
Kati ya maafisa 2500 ambao MSS ilikuwa inatarajia kupeleka Haiti, ni afisa 1000 tu kutoka nchi sita walipelekwa Haiti wakiwemo afisa mia 700 kutoka nchini Kenya.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema kuwa nchi ya Haiti Imepuuzwa na imefadhiliwa vibaya mno huku MSS ikikosa raslimali za kukabili changomoto .
Hali ya kisiasa ya Haiti imekuwa tete tangu rais Jovenel Moise alipouliwa mwaka wa 2021 ilichangia vita pakubwa nchini humo.
Baraza la mpito wa urais lilochukuwa uongozi wa nchi hiyo baada ya mkuu wa mawaziri Ariel Henry kujiuzulu limesema kuwa uchaguzi utafanyika kabla ya mwisho wa mwezi wa Februari mwaka wa 2026.
Kulingana na kamishina mkuu wa haki za kibinadamu, jumla ya watu 3,141 wameuliwa nchini Haiti kufikia nusu ya mwaka huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































