EACC YAFICHUA ONGEZEKO LA HONGO
Idadi ya wakenya wanaotoa hongo ili kuhudumiwa katika idara za serikali ilipanda hadi asimilia 25 mwaka jana kutoka aslimia 17.7 mwaka wa 2023, idara ya polisi ikiongoza katika kupokea hongo.
Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC, asilimia 43 ya waliohojiwa ikikiri kutoa hongo baada ya kuitishwa, asilimia 23 wakiamini kuwa ilikuwa njia ya pekee ya kupata huduma, nayo asilimia 18 ikifanya hivyo ili kurakishiwa huduma.
Idara ya huduma kwa wanyamapori KWS na hazina ya NSSF ni miongoni mwa idara zilizopokea hongo kwa kiwango cha juu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































