#Sports

POLICE FC WAJIANDAA KWA KAGAME CUP

Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya, Kenya Police wameelzea matumaini yao ya kupata ushindi katika robo fainali ya kombe la CECAFA Kagame dhidi ya ya klabu ya Ethiopian Coffee FC, mechi ambayo imeratibiwa kuchezwa leo jijini Dar-es-Salaam, Tanzania.

Akizumgumza kuhusu mechi hiyo, Nahodha wa Police FC David Ochieng maarufu kama Cheche amesema kuwa wamejiandaa vilivyo na wana matarajio makubwa ya kupata ushindi kwani si mara ya kwanza kukutana nao na kupata ushindi dhidi yao.

Police waliambulia alama 3 dhidi ya Garde Cotez na wakapoteza dhidi ya Singida Black Stars na sasa wanashikilia nambari 3 kwenye kundi wakiwa na alama 3, alama 1 nyuma ya nambari 1 na 2 ambao ni Coffee na Black Stars mtawalia.

Imetayarishwa na Nelson Andati

POLICE FC WAJIANDAA KWA KAGAME CUP

KCB RFC NDIO MABINGWA WA KABEBERI 7S

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *