WANDAYI AFICHAU SABABU YA BEI YA MAFUTA KUPANDA
Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amefichua kuwa hakukuwa na fedha katika hazina ya Ushuru wa Maendeleo ya Petroli za kutumika kuwakinga wakenya dhidi ya kupanda kwa bei za mafuta mwezi huu wa Julai.
Wandayi amesema hayo alipofika mbele ya Kamati ya nishati katika bunge la Kitaifa, ambapo ameeleza kuwa serikali ilihitaji bilioni 2.5 kutoa ruzuku kwa bei ya pampu, ila fedha hizo hazikuwepo.
Huu ni mwezi wa pili, tangu Oktoba mwaka jana, wakati ruzuku haikutumika.
Licha ya kushinikiza kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta kabla ya uchaguzi wa 2022, utawala wa Kenya Kwanza umesimamia matumizi ya ruzuku ya mafuta mara kadhaa, kama vile kipindi cha mwezi Aprili-Mei 2025.
Kuhusu masuala mengine yanayohusiana na mafuta, Wandayi ameeleza kuwa bei ya pampu itashuka hivi karibuni, akitaja ongezeko la hivi majuzi la Ksh8 kama hali ya mara moja
Imetayarishwa na Maureen Amwai
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































