SERIKALI YAWATAFUTIA SOKO WAKULIMA MAREKANI
Wakulima nchini sasa wanatarajia kufaidika kutokana na kupanua
kwa fursa za mauzo ya nje baada ya waziri wa Kilimo na maendeleo ya
mifugo Mutahi Kagwe kuanza ziara yake ya wiki moja yenye dhamira ya
biashara nchini Marekani.
Kwenye ziara hiyo, Waziri Kagwe analenga kuwatafutia wakulima soko la moja kw amoja nchini Marekani na kuwaondoa maawakala ambao huwapuinja wakulima.
Tayari Kagwe na ujumbe wake wamefanya kikao na mfanyabiashara mkubwa Walmart anayemiliki maduka ya reja reja zaidi ya 40000 nchini humo, wakilenga kupata fursa za uuzaji wa majani chai, makadamia na mazao mengine.
Afisa mtendaji wa shirika la ustawi wa majani chai KTDA Geoffrey Kirundi na
Wilson Muthaura pia wamepigia debe uwezo wa Kenya kupakia majaini chai mashambani na hivyo kuhakikisha ubora.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































