RUTO: TALAKA NA UCHINA HAIPO
Rais William Ruto ametangaza kwamba hatakatiza uhusiano wa kidiplomasi kati ya Kenya na Uchina na mataifa mengine ya mashariki, baada ya Marekani kutangaza kuangazia upya uhusiano wake wa karibu na Kenya kama mshirika wake asiye mwanachama wa muungano wa NATO.
Katika kikao cha kibiashara jijini Nairobi, Rais Ruto amesema uhusiano wa Kenya na mataifa mengine unachochewa na maslahi yake ya kibiashara, akisema Kenya inafaidika pakubwa kutoka Uchina ikilinganishwa na Marekani.
Marekani imeratibiwa kuchunguza mikataba kati ya Kenya na Uchina, Iran na Urusi, na baadhi ya maafisa wa Kenya kuhusu uhusiano wao na kundi la wapiganaji la RSF nchini Sudan.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































