UBOVU WA BARABARA WAWAHAMISHA WAKAZI
Wakaazi wa Syokimau kaunti ya Machakos wanakabiliana na hali mbaya ya barabara inayosababisha msongamano barabarani na kuharibu magari yao huku seneta wa Machakos Agnes Kavindu akiitaka Seneti kuingilia kati na kushughulikia swala hilo.
Haya yanajiri huku wamiliki wa nyumba wakilazimika kuhamia kwenye nyumba za kukodi jijini Nairobi ili kujiepusha na barabara mbovu na msongamano.
Miongoni mwa barabara zilizoathirika ni ile ya Kiungani,Mwananchi,Community na Parliament, ambazo ziko chini ya Mamlaka inayosimamia Barabara za Mijini KURA.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































