#Local News

SIKU KUBWA YA MUUNGANO WA UPINZANI

Muungano wa upinzani umeratibiwa kutangaza jina na nembo yake rasmi hii leo utakaotumia katika chaguzi ndogo za mwezi Novemba na uchaguzi mkuu ujao huku ukisisitiza kuwa utamteua mgombeaji mmoja atakayemenyana na Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kulingana na viongozi wa muungano huo wakiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, mashauriano yanaendelea katika juhudi za kumtambua mwaniaji mwenye uwezo wa kumbandua rais Ruto kutoka mamlakani kwenye uchaguzi huo.

Haya yanajiri huku mgawanyiko ukiripotiwa ndani ya muungano huo hasa kuhusiana na uteuzi wa Dakta Mukhisa Kituyi kuwa msemaji wake.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SIKU KUBWA YA MUUNGANO WA UPINZANI

MAAFISA 8 NAKURU KUHOJIWA NA EACC

SIKU KUBWA YA MUUNGANO WA UPINZANI

WAKENYA WAMWOMBOLEZA MBUNGE WA ZAMANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *