NPS YATHIBITISHA KIFO CHA AFISA ALIYEPOTEA HAITI

Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) imethibitisha kifo cha afisa wa polisi wa Kenya aliyepotea nchini Haiti wakati akihudumu chini ya kikosi cha kimataifa cha usalama kinachoongozwa na Kenya.
Katika taarifa iliyotolewa hii leo NPS imesema kwamba Benedict Kabiru alipotea tarehe 25 Machi 2025 baada ya kushambuliwa kwenye barabara kuu ya Carrefour Paye-Savien eneo la Pont-Sondé katika jimbo la Artibonite.
Baada ya miezi kadhaa ya jitihada za uokoaji na utafutaji, afisa huyo ametangazwa rasmi kuwa amefariki dunia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna