EPRA YAFUNGA VITUO 10 VYA MAFUTA KUTOKANA NA UCHAKACHUAJI

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) imefunga vituo 10 vya mafuta nchini kwa kuuza mafuta yaliyochakachuliwa au yanayopaswa kusafirishwa nje ya nchi kati ya Julai na Septemba 2025.
Hatua hiyo ilifuatia majaribio 6,090 yaliyofanywa katika vituo 1,315, huku 1,303 zikipatikana zinafuata kanuni. Vituo vingine viwili vilifeli majaribio—kimoja kipo mahakamani, huku kingine kikiendelea na kazi baada ya kulipa faini na kuboresha bidhaa zake.
Kama ilivyoripotiwa, ukiukaji ulijumuisha uuzaji wa dizeli yenye salfa nyingi na mafuta yaliyochanganywa na mafuta ya taa. Vituo vilivyoathiriwa vilikuwa katika kaunti za Nakuru, Uasin Gishu, Kisumu, Machakos, Makueni, Bungoma, Vihiga, Nyandarua, Kwale, Kilifi, Meru, na Mombasa.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi