LAGAT APATA PIGO MAHAKAMANI

Ni pigo kwa naibu Inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat baada ya mahakama kukataa kutupilia mbali kesi inayomshinikiza aondolewe afisini.
Katika uamuzi wake, jaji Chacha Mwita amesema mahakama kuu ina mamlaka ya kikatiba kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusu masuala ya kikatiba yaliyo kwenye kesi hiyo.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanaharakati Eliud Matindi, akitaka Lagat aondolewe afisini kutokana na mauaji ya mwalimu na bloga Albert Ojwang katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa