#Local News

SERIKALI YAPAMBANA KUWAREJESHA NCHINI WANAHARAKATI

Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen ametoa hakikisho kuwa wizara ya masuala ya kigeni inafanya juhudi za kuwarejesha nchini wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo wanaodaiwa kutekwa nyara nchini Kampala walipokuwa kwenye msafara wa kampeni za mwaniaji wa urais nchini humo Robert Kyagulani maarufu kama Bobi Wine.

Hakikisho la Murkomen limejiri baada ya mashirika ya haki za kibinadamu yakiongozwa na chama cha wanasheria LSK kuandika barua ya Pamoja kwa balozi wa Uganda nchini Eunice Kigenyi, wakitaka kuachiwa huru kwa wawili hao mara moja.

Aidha, wameshinikiza uchunguzi kufanywa katika visa vya utekaji nyara wa raia wa kigeni katika mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SERIKALI YAPAMBANA KUWAREJESHA NCHINI WANAHARAKATI

NPS: TUTAHAKIKISHA MAKURUTU WANASAJILIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *