CITY THUNDER WANGURUMA
Licha ya kuwa nafasi moja waingie katika fainali ya Ligi Kuu ya Kitaifa ya Mpira wa Kikapu ya Wanaume, kocha mkuu wa Nairobi City Thunder Brad Ibs amekiri kwamba haikuwa rahisi kuwapita Equity Dumas katika mchujo wa nusu fainali.
Thunder, ambao hawajashindwa msimu huu, wanaingia fainali baada ya ushindi wa 2-0 katika mchujo wa nusu fainali unaochezwa katika msururu wa hatua ya tano bora kwenye uwanja wa Nyayo Gymnasium.
Thunder walishinda Mchezo wa Pili kwa vikapu 69-66 siku ya Jumapili usiku, siku mbili baada ya kushinda Mchezo wa Kwanza 79-77 uliokuwa ukiwaniwa sana dhidi ya Wanabenki.
Kwa upande wake, kocha mkuu wa Equity Dumas Carrey Odhiambo hakufurahishwa na tabia ya wavulana wake katika mechi yao ya mwisho, haswa kuelekea mwisho wa mchezo ambao anaamini uligharimu ushindi.
Timu nyingine ambazo zinafuzu kwa fainali ni timu za KPA za wanaume na wanawake, ambazo zilishinda 2-0 kila moja katika msururu uliochezwa jijini Nairobi, huku michezo iliyosalia ikipangwa kufanyika Mombasa wikendi ijayo.
Dockers wanahitaji ushindi mmoja pekee ili kufika fainali.
Zetech Sparks na Equity Hawks wametoka sare ya 1-1 katika msururu huo, huku mpambano ukitarajiwa wikendi ijayo huku kila upande ukitaka kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyosalia.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































