WAKENYA WAIBUA MASWALI YA UADILIFU WA TUZO
Wakenya wana hadi Jumatatu wiki ijayo kuwasilisha maoni yao kwa bunge la kitaifa kuhusu uteuzi wa wabunge kadhaa na wafanyakazi wa bunge kupewa tuzo za kitaifa kama mashujaa wakati wa sherehe za Mashujaa za mwaka huu.
Maseneta 11 na wabunge 35 akiwemo John Waluke wa Sirisia, Didmus Barasa wa Kimilili na mbunge wa Tiaty William Kamket, wameteuliwa kupewa tuzo hizo, wakenya wakiibua maswali ya uadilifu dhidi ya walioteuliwa.
Wengi wa wabunge walioteuliwa wana kesi au wamewahi kufunguliwa mashtaka mbali mbali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































