MOMBASA UNITED WAONYESHA MAKALI NSL
Klabu ya Mombasa United imeendeleza rekodi yake ya matokeo ya kuridhishwa katika ligi ya NSL, baada ya kuandikisha ushindi wa mabao 2:1 dhidi ya Fortune Sacco kwenye uwanja wa Mbaraki jijini Mombasa.
Mombasa walichukua uongozi katika dakika ya 15 kupitia kwa Emmanuel Gabriel licha ya kukabwa kwa kipindi kirefu na wageni wao, shinikizo zilizosababisha beki wao Felix Ochieng kujifunga.
Hata hivyo, United walirejesha uongozi wao kunako dakika ya 65 kupitia kwa Nehemiah Onchiri.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































