RAIS AJIUZULU KUTOKA WADHIFA ALIOPEWA
Azma ya serikali kuwafidia waathiriwa wa maandamano imepata pigo jingine baada ya Rais wa chama cha wanasheria LSK Faith Odhiambo kujiuzulu kutoka wadhifa wa makamu wa mwenyekiti wa jopokazi lililoteuliwa kuongoza juhudi hizo.
Kwenye waraka wake, Odhiambo ametaja shughuli zilizokwama kutokana na amri ya mahakama huku akisisitiza haja ya marekebisho mapanma ya haki.
Ameongeza kuwa kutokana na shughuli kusimamishwa na mahakama, hakuona haja ya kuendelea kuhudumu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































