KENYA KUADHIMISHA MASHUJAA
Serikali imethibitisha kwamba maadhimisho ya sherehe za Mashujaa zinafanyika hii leo licha ya taifa kuendelea na kipindi cha maombolezo ya Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa serikali Isaac Mwaura amewataka wakenya kujitokeza kwa wingi kuadhimisha sherehe hizo zitakazoongozwa na Rais William Ruto katika uwanja wa Ithookwe kaunti ya Kitui.
Miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa ni Waziri mkuu wa Msumbiji Maria Benvinda Levy na Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































