#Sports

STARS MBIONI KUREJESHA NYOTA

Timu ya taifa ya soka Harambee Stars imeonyesha imani ya kuibuka na ushindi katika mechi zake 2 zilizosalia kabla ya kuaga rasmi kinyang’anyiro cha kufuzu kombe la dunia mwaka ujao litakaloandaliwa katika mataifa ya Marekani, Mexico na Canada.

Stars watamenyana na Burundi Alhamisi hii jijini Bunjumbura kabla ya mechi ya mwisho jijini Abidjan Ivory Coast dhidi ya wenyeji ambao pia ndio viongozi wa kundi F katika uwanja wa Alassane Ouattara Jumanne ijayo.

Nahodha Michael Olunga amesema wako tayari kupata ushindi katika mechi hizo, kauli yake ikisisitizwa na kocha mkuu Benni McCarthy.

McCarthy aidha amethibitisha kuwasili kwa wengi wa wachezaji waliotajwa kikosni.

Miongoni mwao ni beki wa klabu ya Walsall ya Uingereza Vincent Harper ambaye amepewa nafasi kwa mara ya kwanza.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

STARS MBIONI KUREJESHA NYOTA

RAIS AJIUZULU KUTOKA WADHIFA ALIOPEWA

STARS MBIONI KUREJESHA NYOTA

KYLLIAN MBAPPE YUKO SAWA, DESCHAMPS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *