RUTO: NITAREJELEA ZIARA YANGU UKAMBANI
Rais William Ruto ametoa wito kwa wakazi wa eneo la Ukambani kujiepusha na siasa za migawanyiko, akiwahimiza kushirikiana na serikali yake ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo eneo hilo.
Rais alikuwa akizungumza hapo jana wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mashujaa, akiahidi kukamilisha miradi yote ya maendeleo ikiwemo maji, barabara na kilimo.
Rais ameahidi kurejelea ziara yake aliyoifutilia mbali wiki jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































