MAHAKAMA UGANDA YATUPILIA MBALI KESI KUHUSU WANAHARAKATI
Familia za wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo zimepata pigo kutokana na uamuzi wa mahakama kuu nchini Ugandan kutupilia mbali kesi iliyoitaka mahakama kuvishurutisha vyombo vya usalama nchini humo kuweka wazi waliko wanaharakati hao.
Kwenye uamuzi wake, jaji Simon Peter Kinube amesema idara ya polisi na jeshi la ulinzi nchini humo walitii maagizo ya mahakama kwa kuiarifu mahakama kwamba hawana ufahamu kuhusu waliko.
Mahakama sasa imewaorodhesha kama watu waliotoweka, nao wanaharakati nchini wakishinikiza kujiuzulu kwa mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































