#Sports

HAALAND AVUNJA REKODI ZAIDI

Hatriki ya Erling Haaland wikendi iliyopita iliiweka timu yake ya Norway katika nafasi nzuri ya kurejea tena katika mashindano ya kombe la dunia baada ya mara ya mwisho kushiriki mwaka wa 1998.

Mshambulizi huyo wa Manchester City alifunga mabao 3 katika ushindi wa mabao 5:0 dhidi ya Israel.

Kwa sasa Haaland amefunga bao katika mechi 10 mfululizo kwa taifa na klabu msimu huu, akifunga katika mechi 11 kati ya 12 za mwisho.

Aidha, amefunga magoli 51 katika mechi 46 kwa timu ya taifa ya Norway, akiwa mchezaji wa kasi zaidi kufikisha magoli 50 kwa taifa lake, akivunja rekodi ya Harry Kane ambaye alifikisha mabao 50 katika mechi 71.

Ushindi huo unawahakikishia Norway uongozi wa kundi I, alama 6 mbele ya Italia katika mechi 6 ingawa Italia wamechza mechi 5.

Imetayrishwa na Antony Nyongesa

HAALAND AVUNJA REKODI ZAIDI

MWONDOANO WA CAF KUCHEZWA MOROCCO

HAALAND AVUNJA REKODI ZAIDI

KMPDU YATAKA KIAMBU IVUNJILIWE MBALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *