#Local News

WABUNGE, DUALE WARUSHIA MANENO

Kikao cha kupata maelezo kuhusu utendakazi wa mamlaka ya afya ya jamii SHA kimesambaratika baada ya wanachama wa kamati ya afya bungeni kuanza majibizano na Waziri wa afya Aden Duale, aliyewatuhumu wabunge hao kwa madai ya kumshurutisha atoe hongo.

Kamati hiyo chini ya uwenyekiti wa mbunge wa Seme Dakta James Nyikali hata hivyo, imemshutumu Waziri Duale kwa madai ya kuitishia kamati hiyo.

Kulingana na Duale, wabunge wanaikosoa SHA baada ya wizara yake kufunga baadhi ya vituo vya wanavyomiliki wabunge hao.

Imetayarishwa na Antony Nyingesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *