SIKU YA STARLETS UGANI NYAYO
Timu ya taifa ya wanawake ya soka Harambee Starlets ina imani kwamba itashinda mechi yao dhidi ya Gambia hii leo katika uwanja wa Nyayo katika mkondo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika ya wanawake WAFCON.
Mlinda lango wa timu hiyo Lilian Awuor amesema timu hiyo ina uwezo wa kukabiliana na Gambia akisema mechi hiyo ya leo ni fursa kwa wengi wao kushiriki fainali za mataifa ya wanawake na kuwa mchezo huo hautakuwa rahisi ila maandalizi waliofanya yatawawezesha kuvuna ushindi.
Chini ya uongozi wa kocha wao Beldine Odemba sasa kenya inashinikiza kurejea katika hatua ya bara kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2016 ilipocheza mara ya kwanza AFCON NCHINI Cameroon.
Starlets watakuwa wenyeji wa mkondo wa kwanza ugani Nyayo, kabla ya marudiano siku 4 baadaye ugani Stade Lat Dior nchini Senegal kutokana na Gambia kukosa uwanja uliofikiwa viwango vya CAF.
The Gambia ambao wanaorodheshwa katika nafasi ya 124 katika jedwali la FIFA, inasaka kushiriki mashindano ya WAFCON kwa mara kwanza.
Kwa upande wao, Starlets wanaorodheshwa katika nafasi ya 140.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































